Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Mick Wallace, mwanasiasa wa Ireland na mbunge wa zamani wa Bunge la Ulaya, jioni ya Jumapili tarehe 26 April 2026 katika uwanja wa Giuseppe Meazza (San Siro) mjini Milan, na wakati wa mechi muhimu kati ya Milan na Juventus, alionekana kuwa ni miongoni mwa watazamaji huku akiwa ameshika bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kwa mara nyingine alitangaza upinzani wake dhidi ya vitendo vya uhalifu vya Marekani na Israel dhidi ya Iran.
Picha ambayo Wallace aliichapisha katika akaunti yake rasmi kwenye mtandao wa kijamii wa X inaonesha wazi uwepo wake katika majukwaa ya uwanja huo huku akiwa na bendera ya Iran; hatua ya kiishara katika moja ya viwanja muhimu zaidi vya Ulaya na duniani kote, ambayo iligeuka kuwa jukwaa la kulaani mhimili wa kile kilichoitwa ugaidi wa Marekani na Wazayuni.
Wallace katika chapisho hilo aliandika:
“Wale wanaotetea sheria za kimataifa na haki za binadamu wanasimama pamoja na Iran. Kinyume chake ni ugaidi haramu wa Marekani na Israel. Aibu iwe juu ya yeyote anayewaunga mkono Marekani na Israel. Ishi milele Iran.”

Maoni yako